SIRI ZA BIBLIA: NDOTO NI MLANGO WA KIROHO
Manage episode 313499860 series 3273506
Ndoto kwa kawaida ya wanaadamu katika ulimwengu wa mwili ni mambo unaunayoyaona wakati umelala mara nyingi ndoto utaota wakati umelala
Aina za ndoto kwa tafsiri za ulimwengu wa kimwili
- Ndoto unaota kwa sababu umechoka sana mara nyingi ukiota hivyo watu na wewe mwenyewe unasema kua ni ndoto tu kwa sababu ni uchovu
- Ndoto unaota kwa sababu una mawazo kwa kitu kinakufanya ukifikirie sana mfano ajira au mke au mume ukiota mara nyingi unasema ni ndoto tu kwa sababu namuwaza sana au unawaza sana
- Ndoto unaota kwa sababu umehadithiwa au kuambiwa kitu Fulani kabla haujalala harafu unaota hivyo hivyo.
Sasa hayo yote ni katika Ulimwengu wa kimwili tuangalie katika ulimwengu war oho ndoto ni nini?
- Ndoto maana yake ni ( Hesabu 12:6)
BWANA akasema, “Sikilizeni maneno yangu: “Akiwapo nabii wa BWANA miongoni mwenu, ninajifunua kwake kwa maono, ninanena naye katika ndoto.
Maana yake kwamba Mungu anaongea na watu wake kwa kupitia ndoto na maono ila watu wengi ukiota unasema ni ndoto tu
Kila ndoto unayoota inawezekana ikawa inakuhusu wewe au ndugu,jirani,mwenza,rafiki au mtu yeyote ambaye Mungu anakuonesha kitu juu yake na ukiwa unafatilia ulichokiota kwa makini unatakiwa uishi katika ndoto au maono yako anayokunesha Mungu
@siri za biblia
www.sirizabiblia.com
+255 758 708 804
--- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/siri-za-biblia/message119 afleveringen