DRC : Makundi ya waasi yatuhumiwa kwa ukatili wa kijinsia dhidi ya raia mbilimo
Manage episode 418882187 series 1220196
Nchini DRC ; familia ya jamii ya mbilikimo , ukipenda wambute kama wanavyo wanavyofahamika nchini DRC, wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukiukaji wa haki za binadamu.
Wanawake na wasichana kutoka jamii hii wengi ni waathiriwa wa vitendo vya ubakaji , vinavyo tekelezwa na wanaume kutoka makundi ya waasi mashariki mwa DRC, visa hivi vina tendwa na wanaume .
Mwezi Aprili mwaka huu kule mkowani Ituri, watetezi wa haki za binadamu walichapisha ripoti ilioashiria namna wasichana na wanawake mbilikimo , wamebakwa na wanapiganaji wa makundi ya waasi.
Hali hii imedaiwa kuchochewa na imani potofu kwamba , ukitenda tendo la ndoa na mwanamke au msichana mbilikimo, huwezi kufariki kwa risasi vitani wala kuambukizwa baadhi ya magonjwa .
Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.
24 afleveringen